MAREKANI-USHIRIKIANO

Biden na Johnson kukutana ana kwa ana katikati mwa mvutano kuhusiana na Brexit

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, wawili hwa wanakutana kwa mara ya kwanza, ili kudhibitisha uhusiano thabiti kati ya nchi zao baada ya Brexit.
Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, wawili hwa wanakutana kwa mara ya kwanza, ili kudhibitisha uhusiano thabiti kati ya nchi zao baada ya Brexit. AFP - NICHOLAS KAMM,TOBY MELVILLE

Rais wa Marekani Joe Biden ambaye yupo ziarani nchini Uingereza anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson, kujadili masuala mbalimbali kuelekea kikao cha viongozi wa mataifa ya G7 hapo kesho.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hawa wanakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza na ripoti zinasema kuwa, rais Biden atamwambia Johnson kuwa asiruhusu tofauti za kufanya biashara na Ireland Kaskazini, zisiathiri mkataba wa amani baada ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Biden ambaye ana asili ya Ireland Kaskazini amekuwa akisisitiza kuwa, mvutano wowote wa kibiashara kati ya Uingereza, Umoja wa Ulaya na Ireland Kaskazini kusihatarishe makubaliano ya amani yaliyopatikana mwaka 1994.

Mbali na suala hilo, viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadiliana kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Uingereza na Marekani, ambayo yalionekana kuyumba wakati wa uongozi wa rais wa zamani Donald Trump.

Rais Biden anafanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kuhudhuria kikao cha viongozi wa G7 watakaokutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa janga la COVID-19.