UJERUMANI-DINI

Unyanyasaji wa kijinsia: Papa akataa kujiuzulu kwa Askofu Mkuu wa Munich

Reinhard Marx alikuwa ametuma barua kwa Papa mwezi uliopita aondolewe majukumu yake, akisisitiza "kushindwa" kwa kanisa Katoliki la Ujerumani dhidi ya "janga la unyanyasaji wa kijinsia".
Reinhard Marx alikuwa ametuma barua kwa Papa mwezi uliopita aondolewe majukumu yake, akisisitiza "kushindwa" kwa kanisa Katoliki la Ujerumani dhidi ya "janga la unyanyasaji wa kijinsia". Lennart Preiss AFP

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis amekataa ombi la kujiuzulu kwa Askofu Mkuu wa Munich, Reinhard Marx, akimpa msaada mkubwa mwanamageuzi mwenye ushawishi ambaye anashutumu kwa kutofaulu kwa Kanisa la Ujerumani dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Matangazo ya kibiashara

"Endelea kama unavyopendekeza, lakini kama Askofu Mkuu wa Munich", ameandika Papa kwa aliomwandikia kardinali huyo, ambaye pia ni sehemu ya kikosi cha walinzi wake wa karibu.

Askofu Mkuu wa Munich amesema amekubali uamuzi wa Papa Francis "kwa kuutii" huku akisema "ameshangazwa" na chaguo la Francis.

"Sikutarajia atachukua hatua haraka, au aamue niendelee" majukumu yangu, ameelezea katika taarifa, akisisitiza kuwa uamuzi huu ni "changamoto kubwa".

Reinhard Marx alikuwa ametuma barua kwa Papa mwezi uliopita aondolewe majukumu yake, akisisitiza "kushindwa" kwa kanisa Katoliki la Ujerumani dhidi ya "janga la unyanyasaji wa kijinsia".