UINGEREZA-USHIRIKIANO

Uingereza na Marekani zakubaliana ushirikiano dhidi ya magonjwa mapya

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uin gerezaBoris Johnson.
Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uin gerezaBoris Johnson. AP - Toby Melville

Uingereza imetangaza kwamba  imekubali kushirikiana na Marekani kupambana na magonjwa mapya kwa kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa na mpangilio wa matibabu duniani.

Matangazo ya kibiashara

"Ili virusi hii iangamiwze mpja kwa moja na kusitisha kuenea kwa magonjwa yajayo, ni muhimu nchi zote duniani zipate teknolojia ya kisasa ya ufuatiliaji na upangaji kutoka Uingereza na Marekani," Waziri wa Afya wa Uingereza alisema siku ya Alhamisi.

"Kupitia ushirikiano huu mpya wa kihistoria na mshirika wetu wa karibu, tunagawana taaluma yetu na ulimwengu, ili kwa pamoja tuweze kuchukua hatua kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko ya baadaye ili kulinda raia kila mahali," ameongeza Matt Hancock.