G7-USHIRIKIANO

Viongozi wa G7 wajadili kuhusu janga la COVID-19 na mabadiliko ya tabia nchi

Wakati viongozi hao wakiendelea na kikao chao, wanaharakati wamesema ahadi ya kutoa chanjo Bilioni Moja, ikiwemo Milioni 500 kutoka Marekani na Milioni 100 kutoka Uingereza, haitoshi.
Wakati viongozi hao wakiendelea na kikao chao, wanaharakati wamesema ahadi ya kutoa chanjo Bilioni Moja, ikiwemo Milioni 500 kutoka Marekani na Milioni 100 kutoka Uingereza, haitoshi. Getty Images - Hugh R Hastings

Viongozi wa mataifa ya G7, yenye uchumi mkubwa duniani wanakutana nchini Uingereza kujadiliana masuala mbambali, kubwa likiwa ni namna ya kukabiliana na janga la COVID-19 na hali ya mabadiliko ya tabia nchi.

Matangazo ya kibiashara

Hiki ndicho kikao cha kwanza cha viongozi hao wanaokutana ana kwa ana tangu kuzuka kwa maambukizi ya COVID-19 mwaka mmoja uliopita.

Viongozi hao kutoka mataifa ya Ufaransa, Marekani, Uingereza, Canada, Italia, Ujerumani , Japan na Uingereza, wanatarajiwa kutangaza kutoa dozi Bilioni Moja ya chanjo za kuzuia maambukizi ya Corona kwa mataifa masikini.

Mwenyeji wa mkutano huu, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amewaambia viongozi wanaokutana katika mji wa Cornwall, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo kuwa, kukutana kwao kunatoa fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19 na kuhakikisha kuwa, makosa yaliyojitokeza hayarudiwi tena.

Wakati viongozi hao wakiendelea na kikao chao, wanaharakati wamesema ahadi ya kutoa chanjo Bilioni Moja, ikiwemo Milioni 500 kutoka Marekani na Milioni 100 kutoka Uingereza, haitoshi.

Wanaharakati wanataka viongozi hao kuonesha uongozi wa kisiasa na kufanya maamuzi yatakayoiafanya dunia kupata chanjo hizo haraka.