Joe Biden yuko Brussels nchini Ubelgiji kukutana na viongozi wakuu wa Ulaya

Le président américain Joe Biden (centre) à Bruxelles en compagnie du Roi Philippe (droite) et du Premier ministre belge Alexander De Croo.
Le président américain Joe Biden (centre) à Bruxelles en compagnie du Roi Philippe (droite) et du Premier ministre belge Alexander De Croo. REUTERS - KEVIN LAMARQUE

Baada ya mkutano wa G7 na ule wa jumuiya ya NATO na kabla ya kuelekea Geneva Uswisi ambako atakutana na rais wa Urusi Vladimir Poutine, Joe Biden anaendelea na ziara yake barani Ulaya katika hatuwa ya pili ya ziara yake iliompelekea hii leo Juni 15 huko Brussels. Baada ya kipindi cha mtangulizi wake Donald Trump mambo ni mengi ya kuzungumza katika kile kinadaiwa kuwa ni kulisafiasha taifa lake baada ya kuchafuliwa na mtangulizi wake.

Matangazo ya kibiashara

Kuna mada nyingi mezani ambazo Joe Biden atakutana na wakuu watano wa taasisi za Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ursula von der Leyen, Charles Michel na Josep Borrell. Viongozi wa Ulaya wana shauku kubwa juu ya kupata mshirika katika Ikulu ya White House ambae watakuwa wazi kuzungumza kila maswala.

Masomo mawili muhimu

Kwa kweli kuna mada mbili kuu muhimu wakati huu, mabadiliko ya hali ya hewa na Covid-19. Kwenye janga hilo, EU ilikataa pendekezo la Joe Biden la kuondoa haki miliki; lakini amewasili akiwa na pendekezo lake la dozi milioni 500 za chanjo ya BioNTech Pfizer kwa utaratibu wa Covax, ambayo inapaswa kumaliza mizozo.

Mengine bado yanahitaji kupangwa, hususan mzozo juu ya ushuru wa chuma ulioletwa miaka mitatu iliyopita na Donald Trump au hamu ya Ulaya ya kuwatoza ushuru wafanyabiashara wa kimataifa pamoja na makampuni ya mitandao.

Mafanikio

Lakini pia kulikuwa na suala la utoaji ruzuku kwa Airbus na Boeing ambayo, tangu utawala wa George W. Bush, imeweka dosari kwa uhusiano wa kibiashara pande zote za Atlantiki. Wajumbe hao bado wamejadili tangu Juni 14 kwenye sura hii na Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, alithibitisha, Jumanne hii, Juni 15 saa sita mchana, makubaliano ya kusuluhisha mzozo huu wa zamani juu ya ruzuku haramu iliyopewa watengenezaji wa ndege.

Upinzani wa Marekani dhidi ya bomba la mafuta la Urusi na Kijerumani ambalo nalo huenda likajitokeza na kuwa swala nyeti katika mazungumzo.