UFARANSA - COVID-19

Ufaransa yaondoa amri ya kutotembea pamoja na ulazima wa kuvaa barakoa

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari. Juni 16, 2021.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari. Juni 16, 2021. AFP - THOMAS COEX

Uvaaji wa wa Barakoa hautakuwa wa lazima tena ukiwa nje kuanzia Alhamisi, Juni 17 nchini Ufaransa, isipokuwa pekee kwenye maeneo ya mikusanyiko. Na amri ya kutotoka nje itaondolewa kuanzia Jumapili ijayo, Waziri Mkuu Jean Castex alitangaza Jumatano, baada ya kupungua kwa maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex amesema uvaaji wa Barakoa utahitajika pekee ukiwa katika maeneo ya msongamano wa watu (foleni, usafirishaji, maeneo yenye msongamano, viwanja ).

Kuondolewa kwa amri ya kutotoka nje hakutazuia utunzaji wa itifaki za usafi kwa maeneo ya umma na tamasha la muziki la Juni 21 na hafla zingine hadi Juni 30 (kuandaa matamasha nje tu na ishara za kizuizi na sio kwenye barabara ya umma, sheria za viwango vya baa , migahawa na kumbi za starehe. Waziri mkuu amezungumza hayo baada ya kikao cha baraza la Mawaziri na Baraza la Ulinzi lililoongozwa na Emmanuel Macron.

Watu milioni 35 wa Ufaransa watakuwa wamepewa chanjo hadi mwishoni mwa  mwezi Agosti

Wapenzi wa mechi ya mpira wa miguu ya Ufaransa na Ureno pia wataweza kutumia fursa hii mnamo Juni 23. Lengo kuu ni kuhakikisha watu milioni 35 wa Ufaransa wamepewa chanjo kamili mwishoni mwa Agosti, huku akiweka wazi kuwa maambukizi yameshuka hadi kesi 3,200 kwa siku kwa wastani zaidi ya siku 7.

Ufaransa ilikuwa moja ya nchi tatu za mwisho huko Ulaya kuweka amri ya kutotoka nje. Ilianza kutumika mnamo Oktoba 30 saa 9:00 jioni kote jijini, kisha ikapelekwa saa 8:00 jioni kwa kipindi cha likizo ya mwisho wa mwaka na msamaha wa Krismasi. Kisha ililetwa mbele hadi saa 6:00 jioni kwa jiji lote kuu mnamo Januari 16, kisha ikarudishwa hadi 7:00 jioni mnamo Machi 20, kisha hadi 9:00 jioni mnamo Mei 19 na mwishowe hadi 11:00 jioni mnamo Juni 9.