Serikali ya Sweden yaondolewa madarakani baada ya bunge kupiga kura kutokuwa na imani nayo

Waziri mkuu wa Sweden Stefan Löfven, September 09 2018.
Waziri mkuu wa Sweden Stefan Löfven, September 09 2018. Claudio BRESCIANI / TT NEWS AGENCY / AFP

Wabunge mia moja themanini na mmoja kati ya mia tatu arobaini na tisa nchini Sweden wamepiga kura kuidhinisha hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu  Stefan Lofven, ambapo  51 hawakujitokeza kushiriki uchaguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema hii ni mara ya kwanza katika historia ya Sweden kwamba kiongozi wa muungano Social Democratic anakuwa na wiki moja ajiuzulu au kuitisha uchaguzi.

Hatua inakuja siku chache baada ya kuibuka mzozo kuhusu udhibiti wa kodi za serikali ulioongozwa na chama cha mrengo wa kushoto na hivyo kuondoa uungaji mkono wake kwa serikali ya muungano wa kitaifa.

Matokeo hayo yanamaanisha kuvunjika kwa serikali ya muungano wa Social Democrat ambao ni wachache na chama cha Kijani Green Party.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo iwapo waziri mkuu ataamua kuondoka madarakani, spika wa bunge atatakiwa kuanza kufanya mazungumzo na vyama mbali mbali ili kuunda serikali mpya.