UFARANSA-UCHAGUZI

Mwanasiasa wa Ufaransa Jean Luc Melenchon asikitishwa na matokeo ya uchaguzi wa hivi majuzi

Jean-Luc Mélenchon, kiongozi wa chama cha La France insoumise, wakati wa kampeini kuelekea uchaguzi wa 2022, alhamisi January 14 2021.
Jean-Luc Mélenchon, kiongozi wa chama cha La France insoumise, wakati wa kampeini kuelekea uchaguzi wa 2022, alhamisi January 14 2021. AFP - BERTRAND GUAY

Mgombea wa Chama cha mrengo wa kushoto, kinachofahamika kama La France Insoumise Jean-Luc Mélenchon ambaye safari hii amedhirisha nia ya kugombea katika uchaguzi wa urais nchini Ufaransa amesema kuwa hatua ya kutofanikiwa kwenye uchaguzi mdogo wa hivi karibuni inaonyesha kuwepo mgawanyiko mkubwa kati ya wafuasi wa chama cha wanamazingira na na chama chake, hali ambayo amesema inatoa mwanya kwa chama tawala cha La republique en marche kupata ushindi.

Matangazo ya kibiashara

Melenchon ameyasema hayo baada ya kufanyika kwa majadiliano ya kisiasa ambayo yamewaleta pamoja wanamazingira na wafuasi wa vyama washirika huko Brittany, Occitanie na New Aquitaine kuelekea duru ya pili ya uchaguzi mdogo itayofanyika siku ya jumapili ijayo.

Katika barua yake mitandaoni Jean Luc Melenchon amemnukuu mmoja wa wanasisa mashuhuri David Cormand, ambaye ameonesha kuwa amejutia matokeo ya uchaguzi mdogo uliopita huku akiwataka wafuasi wa chama chao cha mrengo wa kushoto kufanya jitihada zaidi katika kuhakikisha matokeo ya duru la pili yanafurahisha.

Jean-Luc Mélenchon, amekuwa akiahidi kuleta mabadiliko ya  kimsingi, kuboresha elimu na kutoa furs aya ajira nzuri endapo atafanikiwa katika urais mara baada ya duru ya pili.