UJERUMANI-MICHEZO

Umoja wa Ulaya wakasirikia UEFA, kukataza taa za rangi7 katika mchezo wa Ujerumani na Hungary.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akisalimiana na Rais wa tume ya umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wakati wa Mkutano wa G7
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akisalimiana na Rais wa tume ya umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wakati wa Mkutano wa G7 REUTERS - PHIL NOBLE

Ikulu ya rais wa Ufaransa, imeeleza kusikitishwa na hatua ya shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, kukataza uwanja wa Allianz Arena wa nchini Ujerumani, kuwasha taa za rangi 7 wakati wa mchezo kati ya Ujerumani na Hungary.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa kadhaa ya Ulaya, yamekashifu hatua ya UEFA, ambapo yalitaka nchi kuonesha rangi hizo kupinga kitendo cha bunge la Hungary, kupitisha sheria inayokataza watoto wa shule kufundishwa maudhui ya ushoga.

Rais wa tume ya umoja wa Ulaya, Ursula von de Leyen, amesema sheria iliyopitishwa na Hungary inaenda kinyume na Imani ya umoja huo kuhusu haki za binadamu.

Von der Leyen ameenda mbali na kusema mswada wa sheria wa Hungary ni aibu na kwamba amewaelekeza makamishna wake kuandika barua kwa mamlaka za Hungary katika kueleza wasiwasi wa tume yake pamoja na hofu ya kisheria kabla ya muswada huo kupitishwa kuwa sheria.

Mkuu huyo wa tume ya umoja wa ulaya amesema muswada huo ni wazi unabagua watu kulingana na jinsia yao, pia unaenda kinyume na imani za msingi za umoja wa ulaya na kwamba zinaenda kinyume na suala la utu, lakini pia ni muswada ambao unaenda kinyume na haki za binadamu.

Hata hivyo serikali ya Hungary haijatoa tamko lolote kuhusiana na kauli hii ya umoja wa ulaya.