UFARANSA

Ufaransa yarekodi idadi kubwa ya watu waliochanjwa kwa siku moja

Kuanzia Jumapili, 66% vijana walio na zaidi ya umri wa miaka 18 walikuwa wamepata angalau dozi moja ya chanjo na 51% walikuwa wamepewa chanjo kamili.
Kuanzia Jumapili, 66% vijana walio na zaidi ya umri wa miaka 18 walikuwa wamepata angalau dozi moja ya chanjo na 51% walikuwa wamepewa chanjo kamili. AP - Constantin Gouvy

Karibu watu milioni moja nchini Ufaransa walimiminika mitaani kwenda kupata chanjo dhidi ya Covid-19 Jumanne wiki hii baada ya Rais Emmanuel Macron kutaka kufanya hivyo Jumlatatu jioni, na mapokezi yalikuwa mazuri, hali ambayo inafanya chanjo hiyo kuwa muhimu na watu kuendelea kuwa na maisha ya kawaida katika jamii.

Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya hotuba ya Emmanuel Macron kuhusu utekelezaji wa hatua mpya dhidi ya tishio la mlipiko wa nne, watu 792,339 walichomwa sindano mchana wa siku moja ya Jumanne.

Kuanzia Jumapili, 66% vijana walio na zaidi ya umri wa miaka 18 walikuwa wamepata angalau dozi moja ya chanjo na 51% walikuwa wamepewa chanjo kamili. Kutokana na aina mpya ya kirusi cha Corona cha Delta kuendelea kushika kasi, kirusi ambacho kinaambukia haraka, serikali imechukua hatua muhimu kuongeza taratibu wa kuchanja raia wake.

"Chanjo sio lazima mara moja kwa kila mtu, lakini tutaongeza muda iwezekanavyo ili kushinikiza wengi wenu kupata chanjo," rais wa Ufaransa alisema siku ya Jumatatu. Chanjo kamili, vipimo) kwa vitakuwa vya lazima kuanzia Julai 21 kwa sehemu za burudani na utamaduni ambapo kunakusanyika watu zaidi ya 50, halafu kwenye mikahawa na sekta ya uchukuzi wa masafa marefu kuanzia mwezi Agosti.