UINGEREZA

Uingereza: Johnson ataka uangalifu zaidi wakati vizuizi vya kiafya vinaondolewa

Uamuzi wa Boris Johnson kuamini ufanisi wa chanjo kupunguza idadi ya visa vikali vya COVID-19 na vifo vinavyohusiana na janga, licha ya kuongezeka kwa maambukizo mapya, inaweza pia kuwa mfano kwa nchi zingine kwa njia ya kusonga mbele kwa kuondokana na hatua ya raia kutotembea.
Uamuzi wa Boris Johnson kuamini ufanisi wa chanjo kupunguza idadi ya visa vikali vya COVID-19 na vifo vinavyohusiana na janga, licha ya kuongezeka kwa maambukizo mapya, inaweza pia kuwa mfano kwa nchi zingine kwa njia ya kusonga mbele kwa kuondokana na hatua ya raia kutotembea. Jonathan Buckmaster POOL/AFP

Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson inatarajia leo Jumatatu kuondoa vizuizi vya mwisho vya kiafya ambavyo bado vinaendelea kutekelezwa nchini humo, baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa hatua za kukomesha kuenea kwa virusi vya Corona, ikitoa wito kwa raia kuwa macho, huku ikiwa na imani na chanjo.

Matangazo ya kibiashara

Kile ambacho vyombo vya habari vya Uingereza vimeelezea kama "Siku ya Uhuru" inafungua sura mpya katika vita dhidi ya mgogoro wa kiafya, serikali ya Uingereza sasa inapendelea kufunguliwa kabisa kwa uchumi ulioharibiwa na shida kadhaa zilizosababishwa na janga la COVID-19 tangu mwezi wa Machi 2020.

Uamuzi wa Boris Johnson kuamini ufanisi wa chanjo kupunguza idadi ya visa vikali vya COVID-19 na vifo vinavyohusiana na janga, licha ya kuongezeka kwa maambukizi mapya, unaweza pia kuwa mfano kwa nchi zingine kwa njia ya kusonga mbele kwa kuondokana na hatua ya raia kutotembea.

Huu ni mkakati hatari, kama vile kuona kuibuka aina mpya ya kirusi cha Corona kinachoweza kuhimili chanjo au kurekodi kuibuka tena kwa maambukizi mapya yanayoweza kupunguza shughuli za kiuchumi. Kwa hivyo Boris Johnson ametoa wito kwa raia kuchukua njia ya tahadhari.

"Huu ni wakati sahihi, lakini lazima tuchukue hatua kwa uangalifu. Lazima tukumbuke kwamba virusi kwa bahati mbaya bado viko," kiongozi huyo wa Uingereza amesema katika ujumbe wa video uliorekodiwa siku ya Jumapili.

Uvaaji wa barakoa si lazima tena

Wajibu wa kuvaa barakoa katika maduka na sehemu zingine zilizofungwa umeondolewa tangu usiku wa manane nchini Uingereza, sawa na idadi ndogo ya watu iliyokuwa imewekwa kwa baa na mikahawa.

Pamoja na hatua hii ya mwisho, London inakusudia kuboresha uchumi wa Uingereza, moja ya nchi zilizoathirika zaidi duniani na smgogoro wa kiafya.

Lakini makumi ya maelfu ya maambukizi mapya yaliyorekodiwa kila siku yanaweza kuzuia mipango ya serikali.