UFARANSA

Karim Benzema apatikana na virusi vya Corona

Kilabu ya Real Madrid imetangaz kwamba mshambuliaji wake Karim Benzema amepatikana na virusi vya Corona.
Kilabu ya Real Madrid imetangaz kwamba mshambuliaji wake Karim Benzema amepatikana na virusi vya Corona. GABRIEL BOUYS AFP/File

Mshambuliaji Mfaransa Karim Benzema amefanyiwa vipimo na kukutwa na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, kilabu chake, Real Madrid, kimetangaza Ijumaa katika taarifa ya sauti bila maelezo zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Karim Benzema alishiriki mnamo Juni michuano ya soka ya Ulaya katika timu ya taifa ya  Ufaransa, iliyoondolewa na Uswisi katika raundi ya 16. Alifunga mabao manne wakati wa michuano hiyo.

Karim Benzema mwenye umri wa miaka 33, raia wa Ufaransa, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Juni mwaka jana wa Ligi kuu nchini Uhispania maarufu kama LaLiga.