UFARANSA

Emmanuel Macron kuzuru kwa mara ya kwanza Polynesia ya Kifaransa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Daniel Cole POOL/AFP/File

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajia kuzuru Polynesia ya Kifaransa, eneo la ng'ambo la Ufaransa katika Pasifiki ya kusini. Katika ziara hiyo, rais wa Ufaransa anatarajiwa kuzungumzia maswala mengi, kama vile nyuklia au COVID-19.

Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Élysée inaiona ziara hii kama hatua mpya katika mzunguko wa Ufaransa aliyoanzisha rais Emmanuela Macon. Miezi nane kabla ya uchaguzi wa urais, rais Macron anafanya ziara katika eneo hilo kwa mara ya kwanza, kilomita 16,000 kutoka mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Emmanuel Macron anatarajia kukabiliana na maswali magumu kuhusiana na COVID-19. Wakaazi wa Polynesia wanasita zaidi juu ya chanjo ya COVID-19 kuliko mahali pengine. Theluthi tatu tu ya wakaazi wa eneo hilo wamepokea dozi ya kwanza dhidi ya COVID-19.

Mara tu atakaposhuka kwenye ndege, rais Macron atazuru kitengo cha COVID katika hospitali ya Polynesia akiwa na ujumbe: "tufanyiwe chanjo! "

Emmanuel Macron, hata hivyo, atazuru Visiwa vya Marquesas - mara ya kwanza kwa rais wa Ufaransa kuzuru eneo hilo.