ITALIA

Maelfu waandamana Ulaya kupinga vizuizi vya Covid-19

Mji wa Naples, moja ya miji mikubwa ya Italia, umeendelea kurekodi visa vya maambukizi ya virusi vya Corona.
Mji wa Naples, moja ya miji mikubwa ya Italia, umeendelea kurekodi visa vya maambukizi ya virusi vya Corona. AFP

Maelfu ya raia wa Italia waliandamana kote nchini Jumamosi dhidi ya hatua mpya zinazowakabili watu ambao hawajachanjwa kupunguza kasi ya maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

"Uhuru!" na "Hapana udikteta" waliimba waandamanaji kutoka mji wa Naples kusini, hadi mji wa Turin kaskazini, wakati huko Milan, waandamanaji walitoa maneno ya kupinga sheria dhidi ya COVID.

Wengi wa waandamanaji hawakuwa wamevaa barakoa.

Kuanzia  Agosti 6, watu watahitajika kutoa uthibitisho wa chanjo, matokeo yanayothibitisha kutoambukizwa virusi hivyo ama ushahidi wa kupona baada ya maambukizo ili kuweza kushiriki katika dhifa za chakula za ndani ama kuingia katika makavazi na mabwawa ya kuogelea miongoni mwa maeneo mengine ya umma

Zaidi ya watu elfu 3 walishiriki maandamano hayo ya  cheti cha kidigitali cha Corona cha Umoja wa Ulaya kinachojulikana nchini humo kama pasi ya kijani .

Hivi karibuni, serikali ya Italia imeimarisha hatua za kupambana na ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi vya Corona, huku ikiweka masharti makali kwa mikusanyiko hasa kwenye viwanja vya ndani