AUSTRALIA

Jeshi kusaidia katika utekelezaji wa vizuizi vya kudhibiti Corona Sydney

Janga la Covid-19 Australia: mbele ya kituo cha chanjo huko Sydney ambapo hatua za kiafya zilimarishwa Jumapili hii, Julai 18. Karibu 11% ya raia wa Australia wamepewa chanjo kamili.
Janga la Covid-19 Australia: mbele ya kituo cha chanjo huko Sydney ambapo hatua za kiafya zilimarishwa Jumapili hii, Julai 18. Karibu 11% ya raia wa Australia wamepewa chanjo kamili. REUTERS - JANE WARDELL

Jeshi la Australia litasaidia polisi kutekeleza vizuizi vya kukabilina na kusambaa kwa virusi vya Corona katika mji mkuu wa nchi hiyo Sydney, wakati mji huu wenye wakaazi milioni sita umerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona Alhamisi wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya hatua kali zilizochukuliwa kukabiliana na janga hilo tangu kuzuka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona, Delta, mji wa Sydney umrekodi visa 239 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24, idadi kubwa zaidi tangu kuzuka kwa janga hilo ambalo halikuiathiri sana Australia, ambayo kufikia sasa imerekodi vifo 921 kwa jumla.

Mamlaka, ambayo inatarajia hali ya afya kuzorota zaidi, imetangaza kuwa polisi huko New South Wales, jimbo ambalo mji wa Sydney unapatikana, itapata usadizi wa wanajeshi 300 kuanzia Ijumaa wiki hii ili kukagua iwapo hatua hizo zinatekelezwa vilivyo.

Muda wa raia kutotembea uliongezewa kwa mwezi mmoja Jumatano wiki hii katika jiji kubwa zaidi nchini Australia, ambapo kampeni ya chanjo imecheleweshwa kwa muda mrefu kutokana na dozi zilizopo na ambapo chanjo ya AstraZeneca ndio inayotolewa tu kwa watu wazima.