UFARANSA

Ufaransa: maelfu waandamana tena kupinga vizuizi vya Covid-19

Maelfu ya waandamanaji waliandamana katika mjini Paris Jumamosi hii, Julai 31 kupinga vizuizi vya Covid-19.
Maelfu ya waandamanaji waliandamana katika mjini Paris Jumamosi hii, Julai 31 kupinga vizuizi vya Covid-19. AP - Michel Euler

Miji mbalimbali ya Ufaransa imekumbwa tena Jumamosi hii Julai 31 na maanamano kupingwa vizuizi vya Covid-19. Makumi ya maelfu ya wapinzani wa vizuizi vya Covid-19 walimiminika mitaani wakisema hawakubaliani na hatua hiyo. Ufaransa imeendelea kukumbwa na maanamano kwa wikendi ya tatu mfululizo.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkesha wa maandamano hayo, mamlaka nchini Ufaransa ilitarajia kuona watu 150,000 wakiandamana. Jumamosi iliyopita, watu 161,000 na walimiminika mitaani kupinga vizuizi vya kudhibiti kusambaa ugonjwa wa Covid-19 na sera za kuwalazimisha kudungwa chanjo. Siku ya kwanza ya maamdamano hayo, watu 110,000 walishiriki maandamano.

Waandamanaji hao wamekasirishwa na muswada mpya wa sheria unaowalazimisha raia kuwa na hati maalumu ya kudhibitisha kuwa wamechanjwa au kuonesha kwamba  hawana maambukizi ya virusi vya Corona ili waweze kuruhusiwa kuingia kwenye mikahawa na maeneo mengine ya umma.

Katika mji wa Paris, maandamano ya kwanza ya watu elfu kadhaa yalikumbwa na makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi. Kabla ya waandamanaji kuanza, kiongozi wa vuguvugu la 'vizibao vya njano', wanaopinga sera ya kijamii ya serikali, Jérôme Rodrigues, amewashtumu "maafisa wa serikali,  waandishi wa habari kwamba wapo katika kuwauzia ufanisi wa chanjo bila hata hivo kuwa na uthibitisho wowote ”.