Ulaya yakumbwa na maandamano baada ya kurejeshwa kwa hatua za kudhibiti COVID

Maandamano yamekuwa yakishuhudiwa katika baadhi ya mataifa ya bara Ulaya, kufuatia kurejeshwa tena kwa masharti ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Covid-19. 

Waandamanaji wakipeperusha bendera na mabango wakati wa maandamlano ya kupinga hatua mpya dhidi ya Corona huko Vienna, Austria, Novemba 20, 2021.
Waandamanaji wakipeperusha bendera na mabango wakati wa maandamlano ya kupinga hatua mpya dhidi ya Corona huko Vienna, Austria, Novemba 20, 2021. © REUTERS/Leonhard Foeger
Matangazo ya kibiashara

Nchini Austria marufuku ya watu kutotembea yamerejea tena, licha ya waandamanaji kujitokeza katika jiji kuu la Vienna, kupinga hatua hiyo ya serikali.

Wiki iliyopita, serikali nchini humo ilitangaza kuwa watu ambao hawajapata chanjo, hawataruhusiwa kutembea katika maeneo ya umma, wakishtumiwa kwa kusababisha ongezeko la maambukizi.

Maandamano mengine yameshuhudiwa nchini Uholanzi na Ubelgiji, huku waaandamanaji wanaopinga mpango wa serikali, wakikabiliana na maafisa wa usalama.

Nchini Poland, visa vipya zaidi ya Elfu 12 vimeripotiwa nchini humo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 ikilinganishwa na hali ilivyokuwa wiki  iliyopita.

 Nchini Uingereza, watu wenye zaidi ya miaka 40 wameshauriwa kuanza kuweka mipango ya kupokea chanjo nyingine ili kuimarisha kinga ya miili yao.

Mbali na barra la Ulaya, serikali nchini Australia, imetangaza kuwa itaanza kulegeza masharti ya watu kuingia nchini humo.