Ufaransa yaimarisha hatua dhidi ya Covid-19, Ujerumani yarekodi zaidi ya vifo 100,000

Waziri wa Afya wa Ufaransa Olivier Veran katika mkutano na waandishi wa habari akieleza kuhusu hali ya ugonjwa wa COVID-19 nchini Ufaransa na hatua mpya za serikali zinazokuja kupunguza kuenea kwa virusi hivyo, huko Paris, Ufaransa, Novemba 25 2021.
Waziri wa Afya wa Ufaransa Olivier Veran katika mkutano na waandishi wa habari akieleza kuhusu hali ya ugonjwa wa COVID-19 nchini Ufaransa na hatua mpya za serikali zinazokuja kupunguza kuenea kwa virusi hivyo, huko Paris, Ufaransa, Novemba 25 2021. © Thomas Coex/ REUTERS

Kutokana na kuzuka tena kwa janga la Covid-19 barani ulaya, Ufaransa imetangaza Alhamisi hii kuimarishwa kwa hatua za kiafya, bila hata hivyo kuweka marufuku ya kutembea, wakati Ujerumani, iliyorekodi visa vingi vya maambukizi, imevuka kizingiti cha vifo vya watu 100,000.

Matangazo ya kibiashara

Wanasayansi wa Afrika Kusini wametangaza leo Alhamisi kuwa aina mpya ya Covid-19 yenye idadi "ya juu sana" ya mabadiliko imegunduliwa nchini humo.

Ulaya kwa mara nyingine tena imewa kitovu cha janga hili duniani msimu huu, wakati aina mpya ya kirusi cha Corona, Delta inayoambukia kwa haraka, imepunguza ufanisi wa chanjo dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo hadi 40%, kulingana na WHO.

Covid-19 imesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 1.5 katika bara hilo, kulingana na hesabu za shirika la habari la AFP kutoka kwa ripoti rasmi. WHO imeonya kwamba Covid inaweza kuua watu wengine 700,000  ifikapo majira ya baridi.

Kwa jumla, virusi vya Corona vimeua zaidi ya watu milioni 5.16 duniani kote tangu mwisho wa mwaka 2019. WHO inakadiria kwamba kwa kuzingatia vifo vipya vinavyohusiana moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja na Covid-19, idadi ya visa vya maambkizi na vifo vinavyotokana an janga hilo inaweza kuwa mara mbili hadi zaidi ya tatu.

Nchini Ufaransa, ambapo Covid imeua zaidi ya watu 118,000, katika hatua hii inachukuliwa kuwa "hakuna marufuku ya kutembeaau watu kuwekwa karantini", ametangaza Alhamisi hii Waziri wa Afya Olivier Véran.

Nchini Austria, viongozi walichukua uamuzi siku chache zilizopita kuweka kizuizi, hatua kali ambayo haijawahi kuchukuliwa barani Ulaya tangu kuanza kwa kampeni za chanjo.