UFARANSA-SIASA

Jean Castex atoa wito kwa vyama vya siasa kujadili kuhusu uchaguzi

Wakati kirusi kipya cha Omicron kikiendelea kushika kasi nchini Ufaransa, serikali, wagombea na wawakilishi wa vyama vya kisiasa wamekutana Jumanne hii Januari 11 kwa njia ya video kujadili mpangilio wa uchaguzi wa rais.

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex huko Saint-Ouen, kaskazini mwa mji wa Paris, Oktoba 14, 2021.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex huko Saint-Ouen, kaskazini mwa mji wa Paris, Oktoba 14, 2021. AFP - SARAH MEYSSONNIER
Matangazo ya kibiashara

Wasiwasi unazidi kuongezeka miongoni mwa vyama vya kisiasa kuhusu mpangilio wa uchaguzi wa urais na kampeni ya sasa ya uchaguzi. Kwa hiyo serikali imewaalika wagombea na wawakilishi wa vyama kusikiliza mapendekezo yao kuhusu mpangilio wa uchaguzi ujao.

Wawakilishi katika mkutano huo wampendekeza wakati wa uchaguzi kutolewe barakoa za FFP2 zilizosambazwa wakati wa kampeni, visafishaji hewa katika vituo vya kupigia kura. Hata hivyo Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani wamekubali kuwa watatoa majibu ya uhakika.