Habari RFI-Ki

AMISOM lawamani kufuatia ripoti ya UN kuhusu ubakaji wa wanawake na wasichana Somalia

Sauti 09:31
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Uganda wanaounda jeshi la AMISOM nchini Somalia
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Uganda wanaounda jeshi la AMISOM nchini Somalia Reuters

Ripoti iliyotolewa na shirika la kimataifa la Human Rights Watch imewatuhumu askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika huko Somalia AMISOM, kuhusika na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, wanawarubuni wanawake kwa kuwapa chakula kama msaada ili wafanye nao ngono, tuhma ambazo AMISOM imekanusha.