DRC-PAPA WEMBA

Raia wa DRC watoa heshima za mwisho kwa Papa Wemba

Umati wa watu mbele ya jengo la Bunge kwa ajili ya kutoa heshima ya mwisho kwa Papa Wemba, Jumanne, Mei 3, 2016.
Umati wa watu mbele ya jengo la Bunge kwa ajili ya kutoa heshima ya mwisho kwa Papa Wemba, Jumanne, Mei 3, 2016. © RFI/ Guillaume Thibault

Raia kutoka maeneo mbalimbali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameendelea kutoa heshima ya mwisho Jumanne hii kwa siku ya pili mfululizo kwa mwili wa Papa Wemba ambaye alifariki siku kumi zilizopita akiwa jukwaani mjini Abidjan, nchini Cote d'Ivoire.

Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii mfalme wa muziki wa Rumba, Papa Wemba alitunukiwa tuzo ya medali ya mashujaa wa kitaifa. Mwili wake ulisafirishwa katika kijiji alikozaliwa cha Molokai kabla ya kurejeshwa katika jengo la Bunge. Raia wamekua wakiendelea kutoa heshima za mwisho kwa nguli hhuyo wa Muziki wa Rumba katika majengo ya Bunge.

Maelfu ya watu wamefurika mbele ya jengo la Bunge, huku vibao mbalimbali vya muziki vikidumbwizwa, ikiwa ni pamoja na bendi ya Lukumbé na kundi la wapiga ngoma la Sankuru, mji wa Papa Wemba. Umati mkubwa wa watu wameendelea kusubiri ili kutoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza.

"Alikua kwa kweli muimbaji mashuhuri, " amesema mwanamke aliyekuja kutoa heshima zake za mwisho. "Alikuwa mzuri kwa kila mtu. " "Nina huzuni mkubwa, " ameongeza mwingine. "Sikutaka kulia mbele ya umati wa watu hapa... Lakini nina machungu kumuona Papa Wemba katika jeneza", mwanamke mwengine amesema akihuzunika.

"Watu kutoka tabaka mbalimbali" pia wamekuja kwa wingi, kwa sababu Papa Wemba alikuwa mfale wa "kuvaa" mtu maarufu kwa wambenda burudani na watu maridadi, mtu mwengine amesema.

"Awali, watu walisema : watu maarufu kwa mavazi ni majambazi. Papa Wemba, katika muziki, alianzisha kivazi bora! Tunamheshimu, ni baba, tutamkumbuka sana, "amesema mmoja wa mashabiki wake.

Julie, binti ya Papa Wemba, amezungumza hapa kwa niaba ya familia na aliwashukuru wanawake, wanaume, watoto kama wazee, waliokuja kutoa heshima zao za mwisho kwa Papa Wemba: "Baba yangu alikuwa baba wa wote. Alikuwa baba wa dunia! Nia yake ilikuwa ya kutuweka pamoja! Umoja, amani, baba alitaka. Ni vizuri kwa kweli! Nawashukuru tena. "

Pamoja na mvua, foleni ya watu wanaokuja kutoa heshima zao za mwisho kwa Papa Wemba imekua ikiongezeka. Zoezi hili litaendelea hadi Jumatano hii asubuhi.