IRAN-SAUDI-HIJA

Wairani hawawezi kutekeleza Hija Makka

Mahujaji milioni tatu wamekusanyika katika mji wa Makkah mwaka 2011.
Mahujaji milioni tatu wamekusanyika katika mji wa Makkah mwaka 2011. Reuters/Ammar Awad

Mwaka mmoja baada ya tukio la kukanyagana lililosababisha vifo vya maelfu ya mahujaji ikiwa ni pamoja na Wairani 464, Tehran inaamini kwamba "mazingira hayajawekwa sawa" kwa Wairani kutekeleza Ibada ya Hija katika mji wa Makkah mwezi Septemba.

Matangazo ya kibiashara

Iran inaituhumu Saudi Arabia "kupuuzia" Ibada hiyo tukufu kwa Waislamu. Ni mvutano mpya kati ya mataifa haya mawili hasimu.

Wairani hawatokamilisha Hija kubwa katika mji wa Makkah mwezi Septemba, kutokana na kushindwa kwa makubaliano juu maandalizi ya Ibada hiyo kati ya Riyadh na Tehran.

"Mazingira hayajawekwa sawa na muda umeshapita mno" kwa maandalizi ya Ibada hii tukufu, ambayo ni wajibu kwa Mwislam mwenye uwezo kuitekeleza, Waziri wa Utamaduni wa Iran Ali Jannati, amesema. Waziri huyo ameishtumu Saudi Arabia "kupuuzia" Ibada ya Hija.

Saudi Arabia tayari imewaomba Wairani kusafiri katika nchi nyingine kwa kupata viza na imepiga marufu ndege za mashirika ya ndege ya Iran kusafirisha mahujaji katika mji wa Makkah.

Mwaka 2015, zaidi ya Wairani 60,000 walijielekeza katika mji wa Makkah kutekeleza Ibada ya Hijja kubwa. Lakini mahujaji 2,300, ikiwa ni pamoja na Wairani 464, walipoteza maisha kutokana na mkanyagano mkubwa. Wakati huo huo iIran lijibu, ikiwatuhumu viongozi wa Saudi Arabia kuwa ni wazembe.

Pitia: Mkanyagano Makkah: Iran inashikilia rekodi ya kusikitisha ya wahanga

Hali hii inaonekana kutoboresha mahusiano kati ya nchi hizi mbili. Riyadh ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Tehran baada uvamizi katika ubalozi wake mwezi Januari. SaudiArbia pia ilivunja mahusiano yote ya kibiashara na safari za ndege kati ya nchi hizo mbili.

Iran nchi yenye wakazi wengi kutoka dhehebu la Mashia na Saudi Arabia yenye wakazi wengi kutoka dhehebu la Masunni wanapingana katika migogoro yote ya kikanda, hasa nchini Syria, Yemen, Iraq, lakini pia kuhusu Bahrain na Lebanon.