SAUDI ARABIA-IS

Ulimwengu wa Kiislamu wakasirishwa na shambulizi katika mji mtakatifu wa Madina

Mfalme Salman wa Saudi Arabia, akiambatana na baadhi ya viongozi wenye ushawishi mkubwa nchini mwake, Riyadh Desemba 23.
Mfalme Salman wa Saudi Arabia, akiambatana na baadhi ya viongozi wenye ushawishi mkubwa nchini mwake, Riyadh Desemba 23. REUTERS/Bandar al-Jaloud/Saudi Royal Court/Handout

Viongozi wa Kiislamu wamelaani vikali shambulio la kujitoa mhanga lililotokea Jumatatu jioni karibu na Msikiti wa Mtume katika mji mtakatifu wa Madina nchini Saudi Arabia, mahali ambapo vurugu za aina yoyote ni marufuku.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili, ambalo liliwaua walinzi wanne wa usalama, ni moja ya mashambulizi matatu yaliyoikumba Saudi Arabia Jumatatu katika usiku wa siku oja kbala ya mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mashambulizi haya hayajadaiwa kutekelezwa na kundi lolote, lakini kwa jinsi yalivyoendeshwa yanakumbusha yale ya wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS), ambao waliendesha mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga, yaliyosababisha vifo vingi nchini Saudi Arabia zaidi ya mwaka uliyopita.

Shambulio la Madina, mji wa pili mtakatifu katika Uislamu baada ya Makka, lilitokea mapema jioni mbele ya Msikiti wa Mtume, eneo linalotembelewa sana na waumini katika siku za mwisho za mfungo wa mwezi wa Ramadhan.

Wizara ya Mambo ya Ndani imebaini kwamba vikosi vya usalama vilikua vikimfuatilia mshukiwa katika kituo cha kuegeshea magari ambapo alikua akielekea katika Msikiti Mkuu. "Wakati ambapo maafisa wa usalama walijaribu kumdhibiti, alilipua mkanda wake, na kuua watu wanne na kuwajeruhi wengine watano," Wizara ya Mambo ya Ndani imesema.

Shambulizi hili limesababishwa hasira kwa viongozi wa madhehebu ya Kisuni na wale wa madhehebu ya Kishia, khadi nchini Iran, hasimu mkuu wa Saudi Arabia katika ukanda huo.