Muziki Ijumaa
Mfahamu Mbilia Bel, mwanamuziki wa kwanza mwanamke kuwika duniani
Imechapishwa:
Cheza - 10:47
Juma hili makala ya Muziki Ijumaa, inakuletea mwanamuziki mkongwe raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, maarufu akifahamika kama Mbilia Bel, leo mtangazaji wa makala haya anakuletea uchambuzi wa kina wa mwanamuziki huyu, yuko wapi hivi sasa, anafanya nini, na muziki wake uko katika hadhi gani hivi leo?Mtangazaji Emmanuel Makundi anaungana na Edmond Lwangi Tcheli kukuletea yote unayotaka kuyafahamu kuhusu mwanamuziki huyu, mwanamke wa kwanza kupata umaarufu mkubwa duniani kupitia muziki.