Muziki Ijumaa

Wafahamu nguli wa muziki wa Afrika wanaoimba mahadhi ya kiafrika

Sauti 10:22
Mwanamuziki raia wa Zimbabwe, Oliver Mutukudzi, ambaye muziki wake una vionjo na asili ya tamaduni za kiafrika
Mwanamuziki raia wa Zimbabwe, Oliver Mutukudzi, ambaye muziki wake una vionjo na asili ya tamaduni za kiafrika DR

Wiki hii kwenye makala ya muziki Ijumaa, tunawaangazia wanamuziki nguli barani Afrika, ambao kwa karibu robo karne hivi sasa, wanafanya na kuimba muziki wenye vionjo vya asili ya mwafrika.Kwa sasa bara la Afrika lina wanamuziki wachache wa aina hii ambao wanautambulisha muziki wao kwenye jukwaa la kimataifa na hasa wanaoimba na kutumia vionjo vya muziki wa Afrika na tamaduni zake.