FMM-VYOMBO VYA HABARI

FMM yajizuia kurusha picha za mashambulizi ya kigaidi

Nembo ya taasisi ya France Médias Monde.
Nembo ya taasisi ya France Médias Monde. DR

Tangazo: utengenezaji wa habari za mashambulizi ya kigaidiVyombo vya habari vya kimataifa vya Ufaransa ikiwa ni pamoja na RFI, France 24 na Monte Carlo Doualiya, vinavyojumuika katika taasisi ya France Médias Monde, vinajiuliza mara kwa mara juu ya utengenezaji wa habari kuhusu mashambulizi ya kigaidi yanayotokea duniani kote.

Matangazo ya kibiashara

Vyumba vya habari vya vyombo hivyo habari vinaelewa umuhimu wa kile kinachopeperushwa kupitia vituo vyake vya habari mbalimbali (picha, habari zinazochapishwa, sauti au video). Hivyo basi, kwa miezi mingi, vituo vitatu vya taasisi ya FMM ( France Médias Monde) vimekubaliana kutothubutu kurusha picha yoyote au sauti ya propaganda ya kigaidi, kutopeperusha ujumbe wa madai, au unaotajwa kuwa ni wa "kundi" au "shirika" lenye nadharia ya kigaidi hasa kwa makundi yanayodai kuwa yenye mafungamano na dola lisilo kuwepo.

Katika muendelezo wa maamuzi haya ya kupinga kutumiwa, na kama vilivyojikubalisha baadhi vyombo vingine vya habari vya Ufaransa, RFI, France 24 na Monte Carlo Doualiya wameamua toka Jumanne hii Julai 26 kutorusha hewani picha za wahusika wa mashambulizi ya kigaidi kupitia vituo vyao na mazingira ya kidijitali, na kuwakujizuia kutumia majina yao.

Fikra hii katika vyumba vya habari vya taasisi ya France Médias Monde, vinavyochangia pamoja na vyombo vingine vya habari, itaendelea na haja ya haraka ya kuwa makini kila mara kwa kutotumiwa kama njia ya propaganda. Ni wajibu kwa vyombo vya habari vya RFI, France 24 na Monte Carlo Doualiya, ambavyo vinafuatwa katika lugha 15 duniani kote.