UFARANSA-DINI-UGAIDI

Manuel Valls ataka kuzuia ufadhili wa kigeni wa Misikiti

Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls, amesema serikali itazuia kwa muda ufadhili wa kigeni wa misikiti nchini humo kwa sababu ya mwendelezo wa mashambulizi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakishuhudiwa nchini humo.

Katika Msikiti wa Fréjus, wakati wa swala.
Katika Msikiti wa Fréjus, wakati wa swala. DR
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Valls imekuwa ikishtumiwa kwa kushindwa kuzuaia mashambulizi ya kigaidi ya hivi punde yakiwa ni ya Padri wa Kanisa Katoliki Kaskazini mwa nchi hiyo aliyeuawa kwa kukatwa shingo na wanajihadi wa Islamic State.

Waziri huyo Mkuu pia anataka wahubiri wa dini ya Kiislamu nchini humo kupewa mafunzo nchini humo sio nje ya nchi.

Viongozi wa dini ya Kiislamu wamesema siku ya Jumapili watakwenda Kanisani kuonyensha umoja wa kidini lakini pia kuonyesha kuwa wanapinga ugaidi.

Uislam ni dini ya pili kwa waumini wengi nchini Ufaransa ambapo Misikiti 2,500 imejengwa nchini kote.

Viongozi wa Kiislam nchini Ufaransa wamekua wakibaini kwamba Uislam na Ugaidi ni mabmbo mawili tofauti, na Uislam dini ya amani inayokataza maovu na kuamrisha kutenda matendo mema. "Uislam unaharamisha ugaidi na mauaji dhidi ya binadamu yeyote, na yule atakaye kwenda kinyume na yale yanayoamrishwa na dini ya kiislam, basi huyo ameangamia, " wamesema viongozi hao.