UINGEREZA-MUZIKI

Mwanamuziki George Michael afariki dunia

Mwanamuziki kutoka Uingereza George Michael akiwa ukumbini mjini Vienna tarehe 4 Septemba 2012.
Mwanamuziki kutoka Uingereza George Michael akiwa ukumbini mjini Vienna tarehe 4 Septemba 2012. REUTERS/Heinz-Peter Bader/File Photo

Mwanamuziki kutoka Uingereza George Michael amefariki dunia akiwa na umri wa 53, meneja wake ametangaza usiku wa Jumapili hii Desemba 25. Salaam za rambi rambi zimeanza kumiminika kwenye mitandao ya kijamii.

Matangazo ya kibiashara

Mwanamuziki huyo nguli, kutoka Uingereza George Michael amefariki dunia akiwa nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 53, meneja wake ametangaza usiku wa Jumapili tarehe 25 Desemba. "Ni kwa huzuni mkubwa tunathibitisha kwamba mtoto wetu, kaka na rafiki yetu George Michael aamefariki kwa amani nyumbani kwake katika siku ya Krismasi," meneja wa mwanamuzik ameasema katika taarifa yake. Sababu ya kifo chake haijawekwa wazi.

George Michael alipata sifa alipokua akitumbwiza katika bendi ya Wham. Na nyimbo kama Wake Me Up Before You Go-Go, Last Christmas au Careless Whisper , zilipata sifa sana. George Michael alianza kazi yake ya kutumbwiza muziki kwa kupiga gita tangu mwaka 1987. Mwanamuziki huyo nyota wa mitindo ya Pop, ambaye jina lake halisi ni Georgios Kyriacos Panayiotou, aliuza zaidi ya milioni 100 ya nyimbo duniani kote na aliongoza mara kadhaa katika nyimbo zilizojizolea sifa nyingi katika mashindano ya muziki.

Wakati wa tangazo la kifo chake, Sky News kwa haraka ilimtaja kama kama msani ambaye atakumbukwa katika ulimwengu wa muziki, kama vile David Bowie, aliyefariki dunia mapema mwaka huu, amearifu mwandishi wa RFI katika mji wa London, Marie Vivent

Salamu za rambirambi kutoka kwa watu mbalimbali na watu mashuhuri zimeanza kumiminika kwenye mitandao ya kijamii baada ya kifo chak kutangazwa. "Ninahuzuni sana. Nimemkosa rafiki mpendwa, mwenye ukarimu, na msanii mwenye kipaji. Rambi rambi zangu kwa familia yake na kwa mashabiki wake wote, " mwanamuziki kutoka Uingereza Elton John ameandika kwenye Instagram. Mwanamuziki wamitindo ya Rock kutoka Canada, Bryan Adams ameandika kwenye Twitter: "Pumzika kwa amani George Michael. Siamini kilichotokea. mwanamuziki wa ajabu na mtu anayependwa, pia bado kijana unatutoka. "

Mwanamuziki kutoka Uingereza George Michael, kabla ya mkutano na vyombo vya habari katika Royal Opera House mjini London tarehe 11 Mei 2011.
Mwanamuziki kutoka Uingereza George Michael, kabla ya mkutano na vyombo vya habari katika Royal Opera House mjini London tarehe 11 Mei 2011. REUTERS/Stefan Wermuth/File Photo

Hizi ni baadhi ya nyimbo alizocheza