DRC-SANAA

Wanamuziki wawili waliotoweka wapatikana Goma

Mji wa  Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Julai 2016.
Mji wa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Julai 2016. RFI/Leonora Baumann

Wanamuziki wawili Black Man Bausi na Archip Romeo waliokua wametoweka kwa siku kadhaa tangu siku ya Alhamisi walipatikana mapema siku ya Jumatatu asubuhi nje kidogo ya msji wa Goma, mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Wanamuziki hao wangelishiriki katika tamasha la kuhimiza amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa ndugu zao, wanamuziki hao waliteswa kisha kutupwa katika msitu usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu nje kidogo ya mji wa Goma.

Black Man alipelekwa hospitali ambako alipokelewa, huku akipewa huduma za matibabu, amesema kaka yake mkubwa, ambaye aliohojiwa na RFI. Hali yake ni mbaya, ameomngeza Remy Changa.

Watu ambao walimuokota walisema kuwa Black Man alikuwa akipiga kelele kwa msaada. Alikuwa havai nguo hata moja, huku uso wake, kinywa na miguu vikifunikwa. Alipiga kelele kwa msaada, licha ya kuwa kinywa chake kilikua kimefungwa kwa kitamba. Alitumia meno yake ili sauti iweze kusikika.