AFRIKA KUSINI-SANAA

Mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini Johnny Clegg aaga dunia

Nelson Mandela wakati wa tamasha la Johnny Clegg, Frankfurt mwaka 1997..
Nelson Mandela wakati wa tamasha la Johnny Clegg, Frankfurt mwaka 1997.. © Alliance/DPA

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Kizulu nchini Afrika Kusini mwenye asili ya Uingereza Johnny Clegg amefariki dunia. Johnny Clegg alisifika kwa nyimbo zake na mchango wake katika harakati za kupinga ubaguzi wa rangi.

Matangazo ya kibiashara

Meneja wa Johnny Clegg, msanii maarufu wa muziki wa Kizulu, amesema katika taarifa kwamba baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani, msanii huyo aliaga dunia mjini Johannesburg.

Alizaliwa nchini Uingereza, na alikulia Kwa Zulu Natal, akizungumza na kuimba kwa Kizulu.

Aliiunga katika bendi za muziki za aina mbalimbali Juluka na Savuka katika miaka ya 1970 na 1980 kabla ya kuunda bendi yake ya kizazi kipya.

Johnny Clegg alipendwa kwa muziki wake. Lakini alikuwa maarufu sana nchini Afrika Kusini.

Alikuwa mtu mweupe ambaye alikubali kuvunja sheria na kujiunga na bendi za wanamuziki weusi wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi. Wakati huo mchanganyiko kati ya watu weupe na weusi ulikuwa ulipigwa marufuku.

Johnny Clegg alikuwa Mzungu, aliyejifunza kuzungumza na kuimba kwa lugha ya Kizulu.

Aliwaleta pamoja watu tofauti. Alikuwa Mwafrika, daraja kati ya tamaduni katika nchi ambayo ilikuwa bado ikijitahidi kuondokana na tofauti zake.

Muziki ulichangia kuunganisha raia wa Afrika Kusini wakati serikali ya kibaguzi iliagiza mtengano wa watu kulingana na rangi zao.Clegg - na muziki wake alionekana adui wa serikali ya watu wachache weupe.

Moja ya nyimbo zake zilizopata sifa ni “Asimbonanga” (Mandela) "ukiwa na maana "Hatujamuona".