COTE D'IVOIRE-SANAA

Cote d'Ivoire: Mwanamuziki maarufu wa mitindo ya Coupé-Décalé DJ Arafat afariki dunia

DJ Arafat katika sherehe ya Tuzo za Coupé-Décalé Abidjan Oktoba 2017.
DJ Arafat katika sherehe ya Tuzo za Coupé-Décalé Abidjan Oktoba 2017. AFP/Issouf Sanogo

Mwanamuziki maarufu wa mitindo ya Coupé-Décalé nchini Cote d'Ivoire, Houon Ange Didier, anayejulikana kwa jina la DJ Arafat, amefariki dunia Jumatatu Agosti 12 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia Jumatatu hii, shirika la utangazaji la RTI limeandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Matangazo ya kibiashara

Karibu saa tano usiku Agosti 11, wakati nyota wa Cote d'Ivoire DJ Arafat na kundi la marafiki zake waliambatana kwenye safari moja kuelekea Abidjan, mji mkuu wa cote d'Ivoire, marafiki zake wakiwa kwenye pikipiki yeye akiendesha gari lake.

Mita chache tu baadae, aligongana uso kwa uso na gari lililokuwa likiendeshwa na mwandishi wa habari wa Radio ya taifa ya Côte d'Ivoire.

Ajali hiyo ilikuwa mbaya, kama zlivyothibitishwa na picha za gari lake lililoharibikavibaya, picha ambazo zilirushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Video zingine zimeonesha DJ Arafat akilala barabarani, akiwa amepoteza fahamu. Alipelekwa haraka hospitalini. Kulikuepo na Uvumi mwingi kuhusu kudorora kwa afya yake, baadhi walikuwa walisem akuwa alivunjika, wengine alifariki dunia, huku baadhi wakisema kuwa ajali yake ilisababishwa na pombe na madawa ya kulevya ambayo nguli huyo alitumia, madai ambayo yalifutiliwa mbali na Yves Jay Jay, afisa wa mawasiliano wa mwanamuziki huyo.

Awali Yves Jay Jay alikuwa ameweka ujumbe kwenye akaunti yake ya Facebook kuwahakikishia mashabiki wake kuhusu hali yake ya afya.

Kwa mujibu wa Yves Jay Jay, DJ Arafat yuko katikachumba cha uangalizi mkubwa, lakini hali yake ya afya inaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa jarida Ivoirien Life, mwandishi wa habari wa Radio ya taifa ya Côte d'Ivoire bado amelazwa hospitalini. Na afya yake inaendelea vizuri lakini bado yuko chini ya uangalizi.