COTE D'IVOIRE-SANAA

Cote d'Ivoire yajiandaa kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa mfalme wa ‘coupé decalé’ DJ Arafat

Wakati wa maandalizi ya kuaga mwili wa DJ Arafat, Abidjan.
Wakati wa maandalizi ya kuaga mwili wa DJ Arafat, Abidjan. © ISIA KAMBOU / AFP

Wiki mbili baada ya kifo cha mwanamuziki DJ Arafat, kilichotokea baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia Agosti 12, 2019, raia nchini Cote d'ivoire wanajianda leo Ijumaa kutoa salamu zao za mwisho kwa mwanamuziki huyo nguli kabla ya mazishi yake Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Waandaaji wanatarajia kupokea watu wasiopungua 100,000 katika uwanja Felix Houphouet-Boigny na pembezoni mwa uwanja huo mjini Abidjan. Uwanja ambao una uwezo wa kupokea takribani watu 40,000.

Televiseni sita kubwa zitawekwa karibu na uwanja huo ili kuiruhusu umati wa watu kufuata sherehe ya kuaga mwili msanii huyo nyota aliyefariki dunia mnamo Agosti 12. Lakini televiseni kubwa pia zitawekwa katika wilaya mbalimbali za mji huo mkuu wa kiuchumi. Tayari uwanja umefunguliwa ili kuruhusu watu kuweza kufuata sherehe hiyo. Lakini sherehe rasmi itaanza saa kumi alaasiri (saa za Abidjan).

"Uwanja umefunguliwa saa 8 asubuhi," amesema Zoumana Bakayoko, mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya mazishi ya DJ Arafat. Kawaida, sherehe ya kuaga mwili itaanza saa 10 alaasiri na kumalizika Jumamosi saa 12 asubuhi. Kwa watu ambao hawatoweza kufika kwenye uwanja, televisheni kubwa zimewekwa katika wilaya mbalimbali za mji wa Abidjan, akam vile Yopougon, kwenye eneo la Ficgayo, katika wilaya ya Koumassi, televiseni kubwa imewekwa kwenye eneo la Inchallah na karibu na randabauti ya manispaa ya Abobo ".

Ange Di Huon maarufu kama DJ Arafat, msanii maarufu wa cote d'Ivoire alifariki dunia leo baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia Agosti 12, 2019.

Mfalme huyo wa ‘Coupé decalé’ alipoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu hospitalini mjini Abidjan, kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya pikipiki aliyokuwa anaiendesha kugongwa na gari.