DUNIA-UISLAM-RAMADHAN-DINI

Mamilioni ya Waislamu waanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan waanza kwa Waislamu. Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa kusoma sana Q'uran.
Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan waanza kwa Waislamu. Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa kusoma sana Q'uran. © SIMON MAINA / AFP

Mamilioni ya Waislamu duniani kote leo Ijumaa wameanza kufunga kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo hujizuwiya kula na kunywa kuanzia alfajiri hadi jua linapozama takriban siku 30 au 29 kutegemea na muandamo wa mwezi.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi wa Ramadhani ni moja ya miezi mitukufu katika kalrenda ya kiislamu ambao husubiri kwa hamu kubwa na waumni wote wa kiislamu ulimwenguni.

 

Mwezi wa Ramdhani ni mwezi wa kuzidisha upendo, kutoa sadaka na kuwakumbuka wote wale wenye kuhitaji msaada.

Ramadhan huanza mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislam ambapo Waislam wanaamini Kuran Takatifu iliwasilishwa kwa Mtume Mohammad katika karne ya saba mnamo mwezi wa Ramadhan.

Waislamu wanaamini kuwa huu ni mwezi wa kupatiwa msamaha na Mwenye-Enzi-Mungu kwa hiyo huzidisha ibada kwa wingi na kuwa karibu na Mwenye-Enzi-Mungu.

Saudi Arabia mahala kulikozaliwa Uislamu pamoja na nchi kadhaa za Mashariki ya Kati,Ghuba na nchi nyingi za Kiislam ikiwemo Indonesia taifa lenye idadi kubwa kabisa ya Waislamu duniani na Ulaya Waislamu wameanza kufunga leo Ijumaa kutimiza nguzo ya tano ya Uislamu, mwezi ambao aya ya kwanza ya Q'uran iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Ni wakati ambapo Waislamu hutafakari kwa undani kabisa matendo yao, kuwa wanyenyekevu zaidi kwa Mwenye-Enzi-Mungu kwa kufuata maamrisho yake na kuachana na maovu yote alilyoyakataza pamoja na kuweza kujizuwiya na matamanio.

Mfungo huu wa ramadhan umeingia wakati raia katika nchi nyingi wakiendelea kusalia ndani kutokana na janga la Covid-19, ugonjwa ulioanzia nchini China, katika mji wa Wuhan mwezi Desemba mwaka uliyopita.

Raia wengi wanakabiliwa na haki ngumu ya kiuchumi, huku wengi wakiwa wamepoteza ajira kutoka na janga hili.

Ugonjwa wa Covid-19 umeuwa maefu ya watu duniani, huku wengine wakiendelea kuhudumiwa katika hospitali mbalimbali baada ya kuambukizwa virusi vya Corona.