UNESCO-MAENDELEO-ELIMU

UNESCO: Zaidi ya robo milioni ya watoto duniani wakosa elimu

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay, amesema janga la Corona limeathiri zaidi shughuli za elimu na kwamba tatizo hilo la kiafya linaweza kuwa chanzo cha kuwafanya watoto wengi wasirudi shuleni hasa wasichana kutoka familia masikini.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay, amesema janga la Corona limeathiri zaidi shughuli za elimu na kwamba tatizo hilo la kiafya linaweza kuwa chanzo cha kuwafanya watoto wengi wasirudi shuleni hasa wasichana kutoka familia masikini. 路透社。

Takriban wanafunzi milioni 260 duniani walikosa elimu mwaka wa 2018 na janga la Corona linazidi kuchangia  tatizo hilo, shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, utafiti na  tamaduni (UNESCO) limesema.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNESCO, wanafunzi kutoka jamii maskini, walemavu ni miongoni mwa wale wanaoathirika hasa wakati huu ambapo janga la Corona limefanya shule kufungwa na elimu mbadala kuendelea kupitia mtandao.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay, amesema janga la Corona limeathiri zaidi shughuli za elimu na kwamba tatizo hilo la kiafya linaweza kuwa chanzo cha kuwafanya watoto wengi wasirudi shuleni hasa wasichana kutoka familia masikini.

Pia katika ripoti hiyo amesema kwamba nchi nyingi bado zina matendo ya kuwabagua watoto kimasomo, ambayo yanachochea uhasama, ubaguzi na kutengwa.

Amezitaka nchi kuwa na hoja ya kuwekeza elimu kwa kuwajumuisha wote bila ubaguzi, huku akionya kuwa kushindwa kuchukua hatua endelevu ni kitendo kitakachozuia maendeleo kwa jamii.